“Ujumbe Mpya umetumwa na Mwumba wa maisha yote. Ni ujumbe wa kumutyarisha binadamu binafsi na kuwatayarisha watu wa dunia ili waishi na waweze kupenya hatari kubwa itayokabili binadamu. Ni zawadi kubwa katika uso wa haja ya haraka. “

Kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu duniani. Ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwumba wa maisha yote ya kulinza na kuendelesha binadamu. Ina onyo, baraka na maandalizi kwa watu wote wa dunia.

Ujumbe Mpya hauna msingi na dini za utamaduni duniani au mafundisho ya kiroho. Ni zawadi kwa watu wa mataifa yote na imani zote. Ina heshimu ukweli unaodumu katika Ujumbe kuu ambazo Mwumba amewahi kutuma duniani, na sio kama chochote kile ambacho kishawahi kufuniliwa kwa binadamu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ni mawasiliano ya halisi kutoka kwa Mwumba ambao umetumwa ulimwenguni wakati wa mabadiliko makubwa, migogoro na mapinduzi. Ujumbe Mpya unatoa maarifa, hekima na mwelekeo ambao ubinadamu wenyewe hauwezi kutoa ili ukabiliane na changamoto kubwa ambayo kwa sasa inakabiliwa na familia nzima ya binadamu.

Ujumbe Mpya ni jibu ya maombi ya dhati kutoka kwa watu mataifa yote na imani za utamaduni kwa uhuru, usalama na ukombozi. Ni ufunuo mpya kuhusu Kiroho Moja, hifadhi ya dunia na mustakabali ya binadamu na hatima ya binadamu ndani ya Jumuiya kubwa ya maisha ya waangavu katika ulimwengu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umo ndani ya mfululizo wa maandiko matakatifu na mafundisho. Ulifunuliwa katika kipindi cha miaka ishirini na tano. Ufunuo bado unaendelea mpaka leo.

admin

Share
Published by
admin

Recent Posts

Miadi Takatifu

Una hatima ya kukutana na watu fulani katika maishani. Una miadi nao. Wataongozwa kukutana na…

12 years ago

Hatima

Ujumbe Mpya umo hapa kuagiza ubinadamu na kuhifadhi utamaduni wa binadamu. Ni jibu ya maombi…

12 years ago

Ujenzi wa Daraja ya Maisha Mpya

Wakati fulani utakuja kutambua kwamba Ufunuo huu Mpya huko hapa ili kukupatia maisha mapya. Hauko…

12 years ago

Kushuhudia Ufunuo

Mtume yuko dunia. Yeye ameuleta Ujumbe mkubwa kwa binadamu, Ujumbe ambao amekuwa akiupokea kwa zaidi…

12 years ago

Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya

Mungu anaongoza binadamu katika mwelekeo mpya, mwelekeo ambao binadamu hajawai kuupitia. Kwa kuwa dunia imebadilika…

12 years ago

Upendo Mkubwa

  Upendo dunia unadhaminiwa sana, kama mnara wa ufarisi wa binadamu. Upendo huimbwa katika nyimbo,…

12 years ago