Tangazo

Ulivyofunuliwa
Marshall Vian Summers
Katika Boulder Colorado.

Kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa  Mungu duniani.

Umetoka kwa Mwumba  wa maisha yote.

Umetafasiriwa katika  ufahamu na lugha ya wanadamu na Hadhara Kuu ya Malaika inayosimamia dunia hii.

Unaendeleza  mfululizo mkuu wa upelekaji wa taarifa kutoka kwa Mwumba, mfululizo huu  umetokea katika Karne na Milenia.

Ni Ujumbe Mpya wa wakati huu na nyakati zitazokuja.

Unatimiliza Mahubiri Makuu ya awali yaliyopewa na Hadhara Kuu ya Malaika, na pia inafunua mambo yale bado Hadhara Kuu ya Malaika haijafunilia binadamu. Ujumbe huu unafunuliwa wakati huu, kwa sababu  binadamu anakabiliwa na changamoto ya matatizo mazito na hatari ya maangamizo kutoka dunia hii na kutoka ulimwengu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umefunuliwa kutahadhari, kuwezesha, na kutayarisha binadamu – watu  kutoka mataifa yote, dini zote za kidesturi, watu wa makabila yote, vyama vyote, jamii zote na mielekeo yote.

Umefuniliwa wakati wa haja kubwa, wakati wa matokeo makubwa.

Unatayarisha binadamu kuwezana na yale yote bado yeye mwenyewe hajayatambua.

Ni ujumbe wa unabii kwa sababu ujumbe huu unatahadhari binadamu kuhusu Mawimbi Makuu ya Mabadilisho yatakayokuja, na pia kuhusu msimamo wa binadamu katika ulimwengu, hasa kuhusu mawasiliano na mataifa yengine.

Ujumbe Mpya waita upepo wa kiroho ulio ndani ya binadamu wote – Majaliwa  iitwayo  Knowledge, iliyopewa jamia nzima ya binadamu. Katika wakati huu, inahitajika kipaji hiki kitayrishwe, kiimarishwe na kiitwe mbele.

Unazungumzia haja kubwa ya kiroho ya mtu binafsi – haja ya kukuwa na maana, kusudi, na mwelekeo.

Unasemea mahusiano makuu yale binadamu anayoweza kuanzisha na mtu mwengine, mahusiano yanayowakilisha kusudi kuu maishani.

Unasemea mahitaju ya dunia na mahitaji ya siku zijazo. Katika kufanya hivyo, inaleta kusudi na utambuzi, umoja na ushirikiano, hekima na nguvu kwa wote wanaoweza kuipokea, kujifunza, kufuata hatua yake, kuwachangia wengine na kushiriki hekima yake katika huduma kwa watu wengine, kwa familia, na kwa jamii, kwa mataifa na dunia nzima.

Ipokee baraka hii.

Jifunze kuhusu Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu.

Tambua kuwa utadhibitisha kilicho halisi katika mila ya kisasa na utasemea hekima ile tayari wamiliki

Utasemea moyo wako, hata zaidi ya mawazo yako na imani yako na mawazo na imani ya utamaduni wako na watu wako.

Ipokee zawadi hii na uisome kwa uvumilivu, ukichukuwa hatua kwa Knowledge, ukijifunza hekima kutoka kwa Jumuia Kubwa na kutambua nguvu ya Kiroho Moja ya binadamu kuunganisha, kuimarisha na kuandaa binadamu ndio aweze kufahamu na kusafiri katika nyakati ngumu zinazokuja.

Ipokee Ujumbe Mpya katika wito wake wa kuhifadhi na kuimarisha ushirikiano wa binadamu, uhuru na uwajibikaji, kwa ajili bila Ujumbe huu Mpya, binadamu atakabiliwa na upungufu mkubwa na shuka.

Binadamu anakabiliwa na upotevu wa uhuru wake na uhuru wa kujitawala katika dunia hii kwa sababu ya kuingiliwa na vikosi kutoka Ulimwengu.

Bila Ujumbe Mpya kutika kwa Mungu, roho ya binadamu itabakia goigoi, na watu wataishi maisha ya ushindani, kukata tamaa, na migogoro.

Nia ya Mwumbi ni, binadamu aibuke Jumuia Kuu ya waangavu katika ulimwengu kama taifa iliyo huru na inajitawala, taifa imara, taifa inayoshirikiana, taifa inayoweza kuhifadhi tamaduni tofauti ikiheshimu ile nguvu zaidi na dhumuni itakayoweza kutunza familia ya binadamu  kuiendelesha ndio ibaki taifa ya nguvu, kudumisha juhudi, kubaki watendaji na wabunifu.

Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu unatoa nafasi mpya ya maendeleo katika nyakati zijazo, lakini kabla ya binadamu aendele, lazima ajitokeze. Lazima aishi nyakati ngumu zinazokuja na lazima ashinde katika ushindani na mataifa ingine kutoka nje ya dunia kuhusu nani atadhibiti dunia hii na hatima yake.

Kila mtu lazima ambue kwamba ana nafasi kubwa ya kugundua Knowledge  ile Mungu amewapa- ile Knowledge ambayo ina lengo lao, maana na mwelekeo na vigezo vya mahusiano yao yote ya maana.

Kuna Ujumbe Mpya kutota kwa Mungu ya mtu binafsi na kuna Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ya dunia nzima.

Iko hapa sasa.

Imemchukua Mtume muda mrefu kuipokea, kwa maana Ujumbe ni kubwa sana.

Mheshimu basi mmoja ambaye amekuja kuleta ujumbe mpya katika ulimwengu.

Yeye ni mtu mnyenyekevu.

Anamiliki hekima iliyomuhimu kufanya jukumu kubwa kama hii, na alitumwa ulimwenguni kwa ajili ya kusudi hili.

Mpokeeni.

Mwelewe.

Lakini musimutukuze.

Yeye si mungu. Yeye ni Mtume anayeleta  Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu duniani.

Huu ndio huo wakati.

Hii ni fursa kubwa.

Hii ni jibu ya maombi ya watu wote duniani walioomba-kwa njia ya kila dini, kwa kila taifa na utamaduni, maombi ya hekima, nguvu, umoja, uhuru na ukombozi.

Pokea Ujumbe hii Mpya sasa.

Umefika, na umefika saa tu wakati muafaka.