Maandalizi ya kukabiliana na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko.


Mabadiliko Makubwa yanakuja duniani, mabadiliko tofauti na kitu chochote ambacho binadamu kwa ujumla amewahi kuona hapo awali – Mawimbi Makubwa ambayo yanakusanya kwa wakati huu. Kwa kuwa binadamu ameathiri dunia kwa njia nyingi, na matokeo ya athari hiyo inakusanyika sasa – nguvu yake inakusanyika sasa, inakusanyika katika wakati binadami kwa kiasi kikubwa hajui kuihusu na hajajiandaa.

Mawimbi haya Makubwa sio tukio moja peke yake. Sio kitu kimoja kidogo ambacho kinatokea wakati moja peke yake, kwa kuwa binadamu ameweka katika mageuzi nguvu za mabdasiliko ambazo sasa lazima akabiliane nazo kwa muda unaoendelea. Kwa kuwa sasa munaishi katika dunia ya rasilimali ambazo zinapunguka, dunia ambapo hali ya hewa imeathiriwa kwa kiasi kikubwa, dunia ambayo hali ya ikolojia inazorota, dunia ambayo binadamu lazima akabiliane na tarajio ya upungufu mkubwa wa chakula na maji na hatari ya magonjwa katika eneo kubwa, hata ikiathiri mataifa yalio tajiri ya dunia. Mizani sasa imebadilishwa, na fanilia ya binadamu kwa jumla lazima iungane na ikusanyike kukabiliana na mabadiliko haya makubwa.

Katika dunia ambapo idadi ya watu inaongezeka na rasilimali zinapunguka, ubinadamu utakabiliana na uamuzi mkubwa, uamuzi wa msingi ya njia ya kuelekea. Je, mataifa yatashindana na kuwa katika migogoro kwa kupata rasilimali zilizobaki? Watafanya vita na migogoro kuhusu nani ambaye atadhibiti rasilimali hizi na ni nani atamiliki rasilimali hizi? Kwa kweli, vita vyote vikubwa vya historia ya binadamu, vimekuwa mapambano, kwa msingi, juu ya kupata na kudhibiti rasilimali.

Je, mataifa yalio tajiri katika dunia yatasisitiza kuwa staili ya maisha yao lazima ihifadhiwe na hivyo kuingia katika ushindani na migogoro na mataifa ingine, wakizidi kuaziri dunia, wakiiba kutoka kwa maskini wa dunia uwezo wao wa kujilisha ndio staili ya maisha makubwa na ya ustarehe iendelezwe katika mataifa tajiri?

Binadamu ikichagua njia hii, itaingia katika hali ya migogoro ya muda mrefu na hali ya upungufu wa kudumu. Badala ya kuhifadhi na kusambaza rasilimali zilizobaki na kujenga uwezo wa kuishi katika hali ya dunia mpya, binadamu itaharibu kile kilichobaki, na itajiweka katika hali ya umaskini na upungufu, na upotevu mkubwa mno wa maisha ya binadamu na matarajio ya mustakabali usio na matumaini.

Lakini bunadamu ikichangua njia tofauti, kwa kutambuwa hatari kubwa inayohusika kwa kukabiliana na Mawimbi haya Makubwa ya Mabadiliko, ikitambua ukubwa wa ukweli na matukio makubwa ambayo yanaweza kutokoea kwa usalama na mustakabali wa binadamu, basi watu na viongozi wa mataifa na dini walio na hekima wanaweza kutambuwa kuwa ubinadamu ulio tenganishwa utashindwa ukikabiliana na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko. Lakini katika umoja, ubinadamu unaweza kujenga njia mpya, kujitayarisha kwa athari za Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko na kuanzisha ushiriki mkubwa na umoja mkubwa kuliko ule binadamu amewahi kuwa na ufarisi wake hapo awali. Hii itaanzishwa sasa, sio kwa sababu ya kanuni za dini ama maadili ya juu, lakini kwa sababu ya hitaji kubwa yenyewe.

Kwa kuwa ni nini taifa moja inatarajia kutimiza kama dunia inatumbukia katika migogoro na upungufu? Mataifa ya dunia yanategemea mataifa ingine kwa kiasi sasa hakuna anayeweza kuchagua njia ya vita na migogoro bila kuleta janga na upungufu kwa kila mtu.

Pamoja, mutakuwa na fursa kubwa. Mukigawanywa, mutashindwa. Na kushindwa kwenyu kutadumu, na kutaleta hasara kubwa mno – hasara kubwa kuliko vita vyovyote ambavyo vimewahi kutokea hapa duniani, vya hasara kubwa kuliko mgogoro wowote wa binadamu ambao binadamu amewahi kujua.

Maamuzi ni machache, lakini ni ya msingi. Na maamuzi hayo sio tu ya viongozi wa mataifa na taasisi ya dini, ila ya raia wote. Kila mtu lazima achague kama atapigana na kushindana, kama atapinga Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko, kama atapambana na mwengne ili aweze kuimarisha staili ya maisha ambayo anashikilia. Ama atatambua hatari kubwa, na ataungana na mwengine na kuanza kujiandaa kwa athari ya mabadiliko na kujenga aina ya mustakabali iliyo mpya na tofauti?

Kwa kuwa hamuwezi kuimarisha vile munaishi sasa. Hayo mataifa yalio tajiri, wale watu walio tajiri, wale watu ambao wamezoea ustaarabu, wakiona kuwa ni haki yao kutoka kwa Mungu na kutoka kwa maisha – lazima wakuwe tayari kubadilisha vile wanaishi, na kuishi maisha ile siyo ya utajiri, kuishi maisha ya kugawa na wengine, kwa kuwa kushiriki rasilimali zilizobaki itahitaji wafanye hivi.

Matajiri lazima watunze maskini, na maskini lazima wajitunze wenziwe, ama kila mtu atashindwa, tajiri na maskini. Hakutakuwa na washindi jamii ya binadamu ikishindwa. Hakutakuwa na taifa kuu. Hakutakuwa na kabila ama kikundi ama taasisi ya kidini kuu tamaduni ya binadamu ikishindwa. Na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yana nguvu ya kuangamiza tamaduni ya binadamu. Huu ndio ukubwa wake. Hivi ndivyo athari yake itakuwa kubwa na itadumu.

Kwa hivyo, changamoto ya kwanza na inayowakabili ni kukabiliana na changamoto hii – bila kusisitiza kupata suluhisho, bila kupinga ukweli wa kile unajua na kile unaona, bila kulaumu watu wengine ama kutarajia mtu mwengine atafute suluhisho badala yako. Kila mtu lazima awajibike kwa vile anaishi, kwa vile anafikiri, kwa kile anafanya, kwa maamuzi yalio mbele yake sasa, na kwa maamuzi ambayo itabidi akabiliane nayo siku za baadaye. Kila mtu, haswa wale wa mataifa yalio tajiri, lazima wafikirie upya pale wanaishi, jinsi wanaishi na aina ya kazi ambayo wanafanya, vile wanajilisha, na vile wanatumia rasilimali za dunia, vile wanatumia nishati – haya yote.

Huu sio wakati wa kutokuwa na uamuzi kuhusu maamuzi yako ama kujilaumu. Kwa hakika sio wakati wa kufikiri kuwa viongozi wa serikali lazima watatue tatizo kwako, kwa kuwa lazima sasa uangalie maisha yako na hali yako.

Ni kama bili imetolewa kwa binadamu. Binadamu amekuwa akitumia na kukopa kutoka kwa urithi wake wa asili kwa muda mrefu, akiweka kando malipo ya matukiio yake kwa muda mrefu, na sasa bili imetolewa. Sasa matukiio yanaibuka kikamilifu, na matukio ni mengi.

Sasa lazima mukabiliane na yale mumejenga. Lazima mukabiliane na hali yenyu. Lazima mukabiliane na dunia ambayo munaijenga kwenyu wenyewe. Kwa kuwa binadamu amepatanya urithi wake wa asili. Hii dunia iliojaa kibiolojia na iliyo nzuri ambayo Muumba wa maisha yote amewapa binadamu kama dunia yake yenyewe, imenyonywa na kupatanywa na kupotezwa – kupitia uchoyo, kupitia ufisadi, kupitia vita na migogoro, kupitia kutowajibika, kupitia kutojua na ujinga – na sasa matokeo yanaanza kujitokeza. Sio tu uwezekano wa mbali ama tatizo la kizazi cha baadaye.

Hii ndio dunia umekuja kutumikia. Hii ndio dunia umetengeneza. Hii ndio hali ambayo unakabiliana nayo sasa. Lazima ukabiliane nayo. Lazima uwajibike kuwa umechanga sehemu yako ndogo kwa kuijenga. Lazima uitikie uwajibika huu bila aibu, lakini hata hivyo uwajibike. Kwa kuwa katika makabiliano na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko, hakuna mahali pa kukimbia na kujificha. Huwezi tu kufunga virago vyako na uhame ushambani ama kutafuta mahali pa kujificha hadi dhoruba hii ipite, kwa kuwa dhoruba hii itadumu muda mrefu, na hakuna pa kujificha.

Ni Knowledge peke yake ndani yako, akili kubwa ile Mungu ameiweka ndani yako, itakayojua namna ya kukabiliana na hali hii na mabadiliko makubwa ambayo yanatokea kwa binadamu. Ni Knowledge hii ya ndani, hii Knowledge takatifu, ambayo itajua jinsi ya kusafiri katia siku ngumu mbele yako, ndio itajua jinsi ya kupandisha tanga katika maji isiyotulia, kwa kuwa kutakuwa na maji ambayo hayatulii.

Labda mezoea kuishi bila kusumbuliwa na shida kubwa za dunia. Labda umejizuia kwa kiasi fulani ambapo zinaonekana kuwa ni za mbali, ambapo hazionekani kuwa ni shida kwako. Zinaokenaka kuwa ni tatizo la mtu mwengine, tatizo la taifa ingine, tatizo ambayo watu wengine lazima wakabiliane nayo. Lakini insulation hii imeisha. Haiwezekani kuwa hutaathiriwa kwa kiasi kikubwa na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko. Haiwezekani kuwa hayatabadilisha hali yako, labda pia kwa kiasi kikubwa mno.

Kwa asili huwezi badilisha kile kinakuja sasa, lakini unaweza kujitayarisha kukabiliana nacho. Unaweza kubadilisha maisha yako ili uweze kuishi. Unaweza kuitumia ili kuchangia kwa usalama wa watu, kwa kuwa hii ndio sababu umekuja duniani. Katika eneo kubwa, zaidi ya mawazo na imani, kuna ukweli ambao umekuja duniani kwa misioni, kwa kuwa uko hapa kwa dhamira na kuwa Mungu amekutuma hapa duniani kuchangia duniani, katika hali hii ambayo inatokea.

Kwa hivyo, akili yako ikijibu kwa hofu na wasiwasi, kwa hasira – labda unaweza kuchanganyikiwa na kushangaa, labda utahisi kuwa huna nguvu na uwezo kaitka uso wa changamoto hii kubwa – lakini ndani yako, katika eneo ya Knowledge, huu, kwa kweli, ndio wakati wako. Huu ndio wakati ambao wito mkubwa utatoa sauti kwako. Huu ndio wakati ambapo vipawa vyako vikubwa vitatoka mbele, kwa kuwa wewe mwenyewe huwezi kuvifanya vitoke mbele. Lazima viitwe kutoka kwako. Na wito lazima utoke kwa dunia, kwa sababu huwezi kujiita mwenyewe kama wito wenyewe utakuwa halisi. Huwezi kujisisimua kwa maisha makubwa. Kwa kuwa wito lazima utoke nje yako – ukiita vipawa vyako kutoka kwako, ukikuita kwa hali kubwa ya akili na ufahamu na kwa sehemu kubwa ya kuwajibika.

Bila wito huu, utakana na kujaribu kusahau na kubaki mjinga na mpumbavu, ama utapigana na kupambana ili kuhifadhi zile haki ambazo unahisi unazo ama lazima uwe nazo. Utatenda kutokana na hofu na hasira. Utakasirikia wengime. Utakuwa na hofu kubwa mno na utachanganyikiwa kabisa. Utaamini kuwa kitu kitakukomboa, kuwa kuna suluhisho katika upeo wa macho ambayo itafanya shida zote ziende. Hautaona na hautajua na hautajiandaa. Na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yakija, hutakuwa tayari, na utakuwa mdhaifu.

Kwa kweli umeona kuwa asili haina huruma kwa wale ambao hawajajitayarisha. Asili haionyeshi huruma kwa wale ambao hawajajitayarisha wa matukio. Mungu anapenda kukuokoa kutoka kushindwa, migogoro na ugomvi. Hio ndio maana Knowledge imewekwa ndani yako. Mungu anajua kile ambacho kinakuja kwa binadamu. Lakini watu wanabaki vipofu na wajinga na wanajitumbukiza kwao wenyewe. Mungu anajua kuwa ukikosa kujiandaa, ukikosa kuwa na nguvu ya Knowledge, ukikosa kuruhusu vipawa vyako viitwe mbele, ukikataa kuwacha maisha yako ya zamani, na seti ya mawazo na dhana, basi utashindwa. Na kushindwa kwako kutakuwa kubwa mno.

Lakini Knowledge ndani yako iko tayari kujibu. Haiogopi Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko. Kwa kweli, imejitayarisha kwa Mawimbi haya wakati huu wote, kwa kuwa hii ndio hatima yako. Haukukuja duniani tu kuwa mlaji, ama tu kujaza nafasi, kuharibu dunia na kutumia rasilimali zake. Haya sio yale yalikuleta hapa, na kwa roho yako unajua kuwa hii ni ukweli. Lakini kile unajua ni ukweli na kile unafikiri bado sio kitu kimoja. Na ni lazima uzilinganishe na Knowledge na ujifunze Njia ya Knowledge na uchukue Hatua kwa Knowledge ndio iwe mwongozi na mshauri wako.

Utahitaji uhakika huu wa ndani, kwa sababu kutakuwa na mchanganyiko, hasira na migogoro wakati watu wakinyimwa, watu wakihisi kuwa wanatishwa na ulinzi wa wao kila mahali ukiwekwa katika changamoto. Utaona watu na vikundi vikijibu kwa hasira. Utaona mataifa yakitisha ingine, na hii tayari inatokea. Na migogoro mikubwa ambayo yatatokea na hatari kubwa ya vita yatavikwa barakoa ya siasa na dini, lakini kwa kweli migogoro ni ya rasilimali. Ni nani atabaki na rasilimali hizi? Ni nani atadhibiti rasilimali hizi?

Migogoro hii tayari imeanza na inaendelea. Na hatari ya migogoro mikubwa, ya vita kubwa, inakuwa kubwa kila siku. Tayari kuna moto ambao unachomeka duniani, na makaa ya migogoro mikubwa yanawashwa, na hali ya matukio yake imekomaa.

Kwa kweli, ukitaka kulindwa na kupata faida kutokana na mabadiliko ambayo yanatokea, huwezi kubaki katika hali yako ya sasa, katika mawazo yako ya sasa, katika dhana zako za sasa. Lazima kuwe na badiliko kubwa ndani yako, na badiliko hii italetwa na hali ya dunia na kuibuka kwa Knowledge ndani yako. Huwezi kubaki mahali upo kiakili, kisaikolojia na kihisia na kuwa na imani ya kweli ya kuishi na kupata faida kutoka mabadiliko makubwa ambayo yanakuja.

Hii ndio onyo kubwa ambayo Ujumbe Mpya inaeleza. Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yanakuja duniani, na binadamu sasa anakabiliwa na ushindani kutoka nje ya dunia – maingilio kutoka mataifa nje ya dunia ambayo yanataka kupata faida kutoka kwa binadamu iliyo dhaifu na isiyo na umoja, ambao wanataka kupata faida kutoka kwa upungufu wa tamaduni ya binadamu.

Mafundishi ya Ujumbe Mpya yanaeleza ukweli hii kikamilifu. Na sio vigumu kuelewa wakati ambao utawacha ulinzi wako, utaweka kando mapendeleo yako, wakati ambapo utaangalia na macho yalio wazi na utasikiza dunia ndio uweze kuona na kujua.

Lakini, kwa kushangaza, akili ya kawaida sio ya kawaida. Labda watu wamepotea kwa yale wanataka ama yale wanaogopa kupoteza. Wamepotea kwa migogoro yao, malalamiko yao, mapambano yao na hao wenyewe na wengine. Kwa hivyo yale ambayo yako wazi na ya kawaida kuona, kusikia, kujua na kufanya yanapotea – yakishindwa na shughuli za binadamu, tamaa ya binadamu na migogoro ya binadamu.

Bila shaka, binadamu inafika katika kizingiti kikubwa sasa ambayo itaamua hatima yake na mustakabai wake. Ushahidi wa hii uko karibu na wewe, na unawza kuuhisi ndani yako – hisia ya wasiwasi, hisia ya ukosefu wa utulivu, mchanganyiko, matarajio ya hofu. Ishara za dunia zinazungumza na wewe – zinakuambia kuwa mabadiliko makubwa yanakuja, kuwa yako katika mlango wenyu.

Unaweza kuyahisi haya, ukijiruhusu kuyahisi – bila kujaribu kujificha ama kuyatoroka, bila kusisitiza kuwa uwe na furaha na bila shughuli, bila kutafuta mambo yasio na faida ndio akili yako ijae shughuli mingi na iwe distracted ndio usisikie ishara za dunia, wito wa dunia na harakati ya Knowledge ndani yako.

Huu ndio wakati wako. Hii ndio sababu umekuja. Haya ndio matukio makubwa ya wakati wako. Hiki ndicho kizingiti kikubwa ambacho binadamu anakabiliana nacho, kwa kuwa sasa lazima mukabiliane na mustakabali ambao utakuwa tofauti na siku za zamani. Maisha haitaendelea kama vile munavyoijua, bila kupingwa. Binadamu haitapata tu chanzo kiingine cha nishati ama suluhisho la uchawi ili kuimarisha mapendeleo ya wachache.

Kwa kuwa munaishi katika dunia ya upungufu. Yale rasilimali ambayo yanapatia mataifa mali, ulinzi na utulivu yanapungua. Mazingira ambayo munaishi yako katika hali ya shinikizo ambayo inaongezeka kupitia uharibifu wa mazingira, kupitia mabadiliko ya hali ya hewa na kupitia athari mingi ambazo zimetokea kwa muda mrefu ndani ya dunia.

Kwa hivyo, munasimama katika poromoko. Je mutaamua kubaki wajinga na mutapigana na kupambana wakati ujinga wenyu na kukana kwenyu kumeshindwa? Ama mutaamua njia ya ujasiri na hekima kwa kujiandaa na kuruhusu zawadi kubwa kutoka kwa Mungu ya Knowledge iwaongoze?

Kujua maana ya zawadi kubwa ya Mungu, lazima muone ukubwa na kina ya changamoto inayokabili binadamu. Lazima muhisi hitaji ndani yenyu, mukitambua kuwa nyinyu wenyewe hamuna majibu na hata mataifa yenyu na wasomi wenyu na wanasayansi wenyu kwa kweli hawana majibu. Wana majibu ya baadhi ya matatizo. Wanafanya kazi kwa kuandaa binadamu, lakini binadamu yuko nyuma sana kwa kujiandaa kukabiliana na Mawimbi Makubwa ya mabadiliko. Hakuna wakati wa kutosha, na hamuko tayari.

Kwa hivyo lazima muhisi hitaji halisi ndani yenyu kujibu zawadi kubwa ile Mungu amewapa – zawadi tofauti kuliko kitu chochote ambacho binadamu amewahi kupokea hapo awali – kwa kuwa binadamu anakabiliwa na changamoto na tatizo tofauti kuliko kitu chochote ambacho binadamu amewahi kukabiliwa nacho.

Kuona suluhisho, lazima muhisi hitaji. Lazima mutambue hitaji. Lazima mukabiliane na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko. Lazima muanze kuweka pamoja sehemu na ishara ili muweze kuona ile picha ambayo inawaonyesha. Picha hii iko wazi na dhahiri, lakini sio dhahiri kwa wale ambao hawaangali, ambao hawafikirii, ambao hawafanyi ushirika wa msingi ambayo inafaa kufanywa kama unaweza kuona picha kwa uwazi.

Tukio lolote la ujasiri ambalo ni la kubadilisha malengo yako na nguvu yako daima lazima liwe na msingi katika hitaji na shinikizo ya ndani. Katika mazingira ya utilivi ni nadra kwa watu kuendelea katika eneo lolote la maisha. Maendeleo ya kweli lazima iendeshwe na hitaji kubwa mno ya ndani – shinikizo kutoka kwa mazingira na kutoka kwa mahitaji ya dunia na pia kutoka kwa Knowledge ndani yako. Knowledge inakuongoza uwe na ufahamu. Inakuongoza ujitayarishe kisaikolojia, kihisia na kwa matendo kukabiliana na changamoto kubwa ambayo yanakuja sasa, kwa matukio makubwa ya maisha yako na kwa mahusiano makubwa ambayo unafaa kuwa nayo. Lakini mahusiano haya yatatokea tu ukikabiliana na changamoto kubwa ya maisha.

Usijali kuwa wengine hawajibu. Usijali kuwa binadamu inabaki katika hali ya ujinga na upumbavu katika ushindi na migogoro yake. Kwa kuwa wito ni wako. Lazima uwajibike kwa maisha yako na dhamira yako ya kuwa hapa. Wito ni wako. Hauhitaji makubaliano na wengine ili uweze kujibu. Hata kama hii ndio kesi, lazima ujibu. Huwezi kusubiri wengine wakupatie uthibiti kuwa unafaa kujibu, kwa kuwa wakati kila mtu atajibu, kutakuwa na hofu na ugomvi. Kutakuwa na dhiki na migogoro. Hutaki kusubiri hadi wakati ambapo kila mtu anajibu, kwa kuwa kutakuwa na ukosefu wa utulivu.

Lazima ujitayarishe na utayarishe maisha yako. Lazima uimarishe mahusiano yako. Lazima ufunze watu walio karibu nawe- wale ambao wanaweza kusikia na wanaweza kujibu. Lazima uweke kando malengo yako na mapendeleo yako ndio uweze kujibu dunia. Lazima ufikirie upya mahali ambapo unaishi, jinsi unavyoishi na wale ambao uko nao katika swala la ni nani anaweza kusafiri na wewe, ni nani anaweza kujiandaa na wewe na ni nani hawezi. Lazima ufikiri upya kazi yako na umuhimu wake katika mustakabali. Na lazima uyafanye haya yote bila kutiwa moyo na wale walio karibu na wewe ama wakubali na wewe, kwa kuwa hii labda haitawezekana.

Akili yako haitataka kukabiliana na siku za baadaye. Akili yako haitataka vitu vingine kwa sababu akili ni dhaifu mno. Inaendeshwa na hofu na mapendeleo. Lakini kuna akili kubwa ndani yako, akili ya Knowledge. Haiko distracted. Haiko katika hali ya mgogoro. Haiwezi kushawishiwa na dunia ama nguvu yoyote, kwa kuwa inawajibika kwa Mungu peke yake. Hio ndio sehemu yako peke yake ambayo ndio safi na inaweza kutegemewa, ni sehemu yako peke yake ambayo ina hekima. Ina dhamira yako kubwa ya kukuja duniani, na inawakilisha uhusiani wako wa msingi na Mungu, ambao haujapotea katika utenganisho.

Licha ya maono ya dunia hii, licha ya shughuli na mlimbiko na majanga ya dunia hii, bado umeshikamana na Mungu. Mungu amekutuma duniani kutumikia dunia katika wakati wake wa haja kubwa. Hiyo ndio maana wewe uko vile ulivyo. Hiyo ndio maana una asili ya kipekee. Hiyo ndio maana una uwezo fulani ambao lazima utumiwe na udhaifu ambao lazima utambuliwe na udhibitiwe kwa hekima. Kwa kuwa huwezi kuwa mdhaifu na ambivalent ukikabiliana na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko. Yatatoa wito wa nguvu yako ya msingi, na utahitaji nguvu hii ya msingi sasa. Huwezi kuwa mjinga sasa ukikabiliana na ugumu na changamoto ya ukubwa kama huu.

Kwa kweli, Mawimbi Makubwa yanakusanya sasa. Hamuwezi kuyaepuka. Ni makubwa mno na yatadumu muda mrefu sana. Je, una uwazi, unyenyekevu na uaminifu wa kuyaona kikamilifu, kujiandaa kukabiliana nazo kwa kihisia, kisaikilojia na kuanza kujenga msingi wako mwenyewe – msingi ambao umejengwa na Knowledge ndani yako, msingi wa mahusiano, msingi wa shughuli na msingi wa hekima? Unajenga msingi huu sio tu kuweza kusafiri mabadiliko haya makubwa, lakini kuweza kusaidia na kutimikia wengine.

Kwa kuwa lazima ujue kuwa mahitaji ya binadamu yatakuwa makubwa mno katika mustakabali. Kila mtu atakua maskini, na wengi watakuwa katika hali ya umaskini mkubwa mno. Lazima uwe na nguvu hapa sio tu wa kujichunga lakini kuwachunga wengine – kuwachunga wazee, kuwachunga watoto. Kwa kweli wewe mwenyewe hutachunga kila mtu, lakini itakuwa wazi ni nani miongoni mwa majirani wako ama mahusiano yako haswa walio wadhaifu. Lazima uwe na nguvu ya kutosha ya kuwachunga pia hao.

Ingawa hii inaonekana kuwa ni kubwa, ingawa hii sio ile ambayo ungependa kufanya, hii kwa kweli ndio itakukomboa, kwa kuwa hii itakutoa kwa migogoro yako, addictions zako, kutojiamini, majuto yako, kumbukumbu za uchungu. Hii itakulazimisha uimarishe mahusiano ya kweli nawe mwenyewe na wengine na dunia.

Kwa hivyo usiangalie Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko kama tu janga ama hatari kubwa, lakini kama wito, kama hitaji – wito na hitaji ambayo inaweza kukurejesha na kukukomboa, ambayo itaiita mbele Knowledge ndani yako na vipawa vikubwa ambavyo umekuja kuvitoa, vipawa ambavyo vitaamuliwa na hali ambayo sasa inaibuka.

Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yataleta uwazi kwa maisha yako, na yatakuonyesha udhaifu na nguvu zako. Yatakutoa kutoka ndoto zako za utimizo na janga. Yatakuleta kwa hisia zako, na yatakuleta kwa Knowledge ndani yako. Kwa hivyo, usiyakane. Usiyakatae. Usifikiri kuwa hayana maana ama kuwa watu watakuwa na suluhisho rahisi kwao, kwa kufanya hivyo ni kujikana wito na nguvu ya wakati wako na ukombozi ambao unafaa kukuleta kwa wale waliotumwa duniani kwa sababu ya hali hii.

Hii itakuunganisha na nguvu yako, na itavunja muungano wako na udhaifu wako, kwa kuwa ni wewe ambaye lazima aitwe mbele sasa. Hili sio tatizo la wengine la kurekebisha, kwa kuwa kila mtu lazima achangie sehemu yake. Na wengi wakiitwa katika dhamira kubwa hapa, basi nafasi ya binadamu kufaulu itakuwa kubwa, na ahadi ya binadamu itakuwa kubwa na uwezekano wa binadamu kuishi katika Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko na kuanzisha njia mpya na mwelekeo mpya na umoja na ushiriki mkubwa itakuwa kubwa.

Lakini inategemea ile nguvu ulizaliwa nayo, nguvu ambayo sasa lazima itoke mbele kwa Knowledge ambayo Mungu ameweka ndani yako, ambayo peke yake inajua njia mbele.

Kwa kwa nyakati kubwa ziko nayni. Huu ndio wakati wenyu. Huu ndio wito wenyu. Hapa ndipo nguvu yenyu halisi itapatikana. Nguvu halisi kamwe haipatikani kama watu hawajali na wanalala. Hupatikana tu wakati watu wanajibu na wanafanya kazi kwa kupitia mwelekeo halisi na nia halisi.

Na katika Mafundisho ya Ujumbe Mpya, binadamu sasa ina matumaini makubwa. Kwa mara ya kwanza, kiroho kinafundishwa katika eneo ya Knowledge. Ni wito mkubwa. Ni zawadi kubwa. Inaleta nayo hekima zaidi kuliko ile binadamu amewahi kuimarisha. Inaita watu nje ya vivuli – nje ya migogoro, nje ya vigambo, nje ya addictions, nje ya janga – kujibu kwa dunia iliyo na mahitaji.

Kwa kuwa Ujumbe Mpya unazungumzia hitaji kubwa ya dunia – Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko na Giza Kubwa ya maingilio ambayo iko duniani. Unazungumzia dhamira kubwa ambayo imeita kila mtu hapa. Unazungumzia nguvu ya Knowledge na unafunua jinsi Knowledge inaweza kutambuliwa na kuwa na ufarisi wake. Unazungumzia eneo la mahusiano ambayo watu lazima wafikie kama wanataka kupata muungano wa kweli na nguvu na wengine. Unazungumzia mustakabali wa binadamu katika Jumuiya Kubwa ya waangavu ulimwenguni na kizingiti kukibwa ambacho binadamu lazima apitie kupata hatima na utimizo wake mkubwa.

Umebarikiwa, basi, kupokea Ujumbe huu, kufahamishwa kuhusu Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko na kuhusu Giza Kubwa ambayo iko duniani. Kwa kuwa una wakati wa kuwa na ufahamu, kujiandaa na kuandaa maisha yako na kupokea uongozi ambao Mungu amekupatia kupitia Knowledge ambayo ulizaliwa nayo, ambayo ni kipaji kikubwa kutoka kwa Mungu kwako na kwa dunia.