“Upendo mkubwa umeleta Ujumbe huu Mpya katika dunia – upendo wa Muumba kwa maumbile, upendo wa Muumba kwa familia ya binadamu- kuonyesha ubinadamu nafasi yake kubwa ndani ya dunia kuwa taifa ya umoja na iliyo huru.”
Ujumbe Mpya unamilikisha mapenzi na Mungu kwa binadamu, wa sasa na wakati ujao. Mapenzi ya Mungu yametafsiriwa katika lugha, katika maandalizi na katika mafundisho kamili na Malaika ambao wanawakilisha mapenzi ya Mungu na madhumuni ya Mungu kwa binadamu katika ulimwengu huu.
Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu ulitolewa katika kipindi cha zaidi ya miaka 25. Ilitolewa katika hali ya kupokea ufunuo na Marshall Vian Summers.Kila neno la ujumbe lilisemawa na likarekodiwa, halafu baadaye likanukuliwa.Hii imelinda uadilifu na usafi wa Ujumbe Mpya katika fomu yake ya asilia. Kile ambacho hatimaye kilikuwa vitabu nzima kilitolewa katika siku au hata masaa. Kwa mfano, sura 27 za Kiroho kutoka kwa Jumuiya Kuu: Ufunuo Mpya zilitolewa katika siku kumi na moja tu. Utaratibu huu wa ufunuo unaendelea.
Hii ndio jinsi Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu umekuja ulimwenguni, na mfululizo huu unalingana na Ujumbe yote kubwa ambayo yamewahi kumtumwa ulimwenguni kwa maendeleo ya binadamu. Mungu hutoa mawasiliano haya makuu na ya wakati muafaka kwa njia ya Malaika, katika dunia hii na dunia zote ndani ya Ulimwengu. Hii ni hali ya mawasiliano na Mungu. Hii ni jinsi Mungu huwasiliana na watu binafsi na mataifa yote na jamii.
Ujumbe Mpya kutoka kwa Mungu unafaa kutumikia ubinadamu wakati huu na wakati ujao. Ni Ujumbe kubwa sana. Zawadi yake, ufanisi wake na muda wake wa milele kwa familia ya binadamu kamwe usidunishwe.
Inamiliki hekima na maarifa, maarifa na hekima zaidi ya kitu chochote ambacho ubinadamu umeshawahi kupewa. Na itachukua ujasiri mkubwa, unyenyekevu na uvumilivu kupokea kiasi kamili ya maneno ambayo Ujumbe Mpya inamiliki. Nguvu yake, ukweli wake na amani ambayo inyotoa inazidi akili ya binadamu.
Ujumbe Mpya wa Mungu una matumaini na ahadi ya kuongoza familia ya binadamu katika siku zijazo ili binadamu aweze kujenga uhuru na haki kuu katika dunia na kuchukua nafasi yake kama taifa huru na umoja katika Jumuiya Kubwa.