Hatima

Ujumbe Mpya umo hapa kuagiza ubinadamu na kuhifadhi utamaduni wa binadamu. Ni jibu ya maombi isiohesabika kwa uongozi wa mtu binafsi na kuleta ushirikiano mkubwa, nguvu na ubunifu wa familia ya binadamu kwa wakati wake wa haja kubwa na taabu.
Ni kubwa sana, kiasi watu hawataweza kuielewa, ingawa watafikiri wameielewa. Na hata hivyo ni rahisi kiasi watu wanaweza kuitumia leo, katika kila hali, na kwa kila mtu ambaye watakutana naye, katika kila seti ya mazingira.
Ujumbe Mpya ni wa kuandaa binadamu ili aweze kuishi katika dunia mpya na kuandaa binadamu katika mahusiano na maisha iliyo nje dunia hii, ushiriki ulio sehemu ya hatima yenyu na mageuzi.
Wakati huu sasa, ubinadamu hauko tayari kukabili pointi hizi kubwa za mageuko – vizingiti hivi vikubwa ambavyo vitahitaji nguvu zaidi, utambuzi mkubwa zaidi na huruma mkubwa kutoka kwa watu kila mahali.
Ni wito mkubwa wa mtu binafsi awe na hekima na awajibike, awe na uwezo na uelewa. Ni zawadi ya watu wote na mataifa. Ni zawadi ya wakati huu na nyakati zijazo. Unajibu maswali ambayo bado hamujaweza kujifunza kuyauliza. Unatatua matatizo ambayo watu bado hawajafahamu.
Unaleta hekima ya Muumba. Umetumwa na uwepo wa Malaika, ambao unatafsiri mapenzi ya Muumba katika maneno, mawazo na maombi.
Ujumbe Mpya unatoa ufafanuzi wake na mazoezi. Kwa kuwa hauwezi kuachwa kwa watu na watu binafsi, hata wasomi na wataalamu, kuamua maana yake na jinsi mazoezi yafaa kufanywa. Ujumbe Mpya wenyewe unazungumzia mambo haya na unafafanua mambo haya ili upunguze kwa kiasi kikubwa uvumi wa binadamu na tafsiri ya binadamu. Dhumuni ya kufanya hivyo ni kupunguza uwezekano wa makosa ambayo yanajitokeza wakati watu wanashughulika na jambo kubwa ya aina hii.
Tahadhari kubwa inafanywa kutoa mafundisho haya, mazoezi na ufafanuzi- ikisemwa kwa njia nyingi tofauti, ikitumiwa katika hali tofauti, ikionyeshwa tena na tena ili ufafanuzi wake uweze kuwa wazi na kusiwe na ukosefu wa udhahirifu unaohusiana nao.
Kwa mara ya kwanza, Ufunuo Mpya unaotolewa kwa ubinadamu unao uwezo wa kusoma na kuandika, kwa dunia ya mawasiliano ya dunia nzima, dunia ya biashara na kwa baadhi ya watu wengine wanaoanza kufahamu dunia.
Unaotolewa sasa katika kina kubwa na ufahamu ili uweze kuunganisha watu wa tamaduni, temperamenti, raia wa nchi na rangi tofauti ndio uweze kupatikana na kueleweka na mtu binafsi, bila kutegemea wasomi wakubwa au taasisi kuamua nini maana yake, nini inasemwa na jinsi mtu anatakiwa kujibu.
Ujumbe Mpya unatoa wito ili nguvu ya Knowledge iliyo ndani ya mtu binafsi itokee-nguvu iliyo ndani zaidi ya mazingira ya akili, nguvu isiyoweza kueleweka na bado ni sehemu ya ufarisi wako.
Kwa baadhi kadhaa ya watu, hii itakuwa ngumu sana kushughulikia. Wao huangalia kila kitu duniani kama ni rasilimali ya akili zao. Lakini Knowledge ni kubwa sana na haiwezi kutumika kama rasilimali ya akili. Watu ambao wanadai wanafuata Knowledge watakuwa wakifuata mawazo yao. Watu ambao wanaodai wanaongozwa na Knowledge wataongozwa na hali zao za kijamii au na tamaa zao. Na hivyo kwa baadhi ya watu hii itakuwa ngumu sana kuelewa. Hii ni kwa sababu ya jinsi wanavyojiona wenyewe na dunia.
Si kila mtu atakuwa na uwezo wa kufahamu ukweli mkubwa kwa wakati huu. Lakini kama watu wa kutosha wataweza, itatoa ahadi kubwa kwa siku zijazo, na kwa usalama na uhuru wa binadamu.
Dunia mpya itakuwa hatari zaidi kuliko dunia ambayo umezoea. Na Jumuiya Kuu ya maisha ni ya tatanisho na ngumu.
Ni lazima mujifunze kuihusu. Ni lazima mujifunze Hekima na Maarifa kutoka Jumuiya Kuu. Na hiki ni kitu ambacho Mungu pekee  anayeweza kuwafunza. Hata mataifa mengine hayawezi kufanya hivyo, kwa kuwa hawajui akili ya binadamu na roho ya binadamu cha kutosha ili waweze kufanya hivyo na hawadhumuni uhuru, isipokuwa mataifa chache tu.
Umezaliwa katika wakati huu. Umezaliwa kwa sababu ya wakati huu. Ni hatima yako kuwa hapa, kujifunza kuhusu mambo haya. Ni hatima yako kupokea maneno haya. Ni hatima yako kugundua Ufunuo Mpya.
Watu wengi duniani hawajaweza kujitolea katika dini za utamaduni za binadamu kwa sababu kuna kitu katika roho yao kilichowaambia wasubiri. Labda wanahalalisha hii kwa ajili ya mapungufu au matatizo yaliyopo ndani ya mila fulani. Lakini hiyo siyo suala, unaweza kuona, kwa kuwa hatima yao ni kitu kiingine, na ilibidi wasubiri Ufunuo. Si ati kwamba mila yao ni duni kwa jinsi fulani. Ukweli ni hatima yao ni kitu kiingine kwa sababu ya asili yao na vile walivyoumbwa, kwa sababu ya dhamira yao, kwa sababu ya hatima.
Hii ni nguvu kubwa kuliko akili ya binadamu, na inaleta changamoto zake zenyewe na baraka zake kubwa na fursa.
Njia ya kurudi kwa Mungu sio ya kiakili. Huwezi kuja kwa Mungu kwa njia ya madai yako. Ukweli na uumbaji havipo kulingana na uelewa wako au tathmini. Mawazo yako hayana madhumuni mbinguni, ni ushiriki wako peke yake.
Hatima si kitu ambacho unaweza kuagiza mwenyewe, wala kitu unaweza kufafanua na kusema, “Hii ni hatima yangu kwa sababu nilalipenda wazo hilo.”
Hatima inahusu pale ulipotoka na pale utaenda na sababu yako kuwa hapa duniani na pale dunia inaenda-mambo yalio zaidi ya mazingatio na ufahamu wa watu.
Hatima itakuongoza, kwa kuwa ni sehemu ya Knowledge iliyo ndani yenu-akili kubwa ambayo Mungu amewapa, iwaandae na iwalinde, iwafafanulie njia yenu na iwashiriki na hatima yenu.
Watu wa Ufunuo Mpya ni sehemu ya kizingiti mpya cha maelewano kwa binadamu kwa sababu binadamu anaingia katika dunia mpya- ulimwengu wa mabadiliko ya mazingira; ulimwengu wa ukosefu wa utulivu wa kisiasa na kiuchumi; ulimwengu wa rasilimali utovu; dunia ambapo hatari ya mgogoro ushindani, na vita itakuwa kubwa sana; dunia ambayo inahitaji ushirikiano mkubwa na hali ya hatima moja pamoja na wengine.
Bila umoja, ubinadamu utashindwa katika Jumuiya Kubwa na kuanguka chini ya ushawishi wa nguvu za kigeni, kama vile ilivyojitokeza mara mingi katika historia ya ulimwengu. Hiyo ni hatari kubwa kwenyu.
Hata hivyo, ni nani ambaye anayatambua haya? Ni nani ambaye anayawaza mambo haya? Ni nani ambaye ana wasiwasi kuhusu haya? Yale watu wanayafikiri na, wanaamini na wanatarajia ni tofauti sana yale Mungu anajua, na hapa ndipo lazima daraja ijengwe. Hii ndio maana Mungu ameiweka Knowledge ndani yako-ili uweze kupata uelewa huu mkubwa na kubainisha ukweli mkubwa.
Mungu ametoa Hatua kwa Knowledge kushiriki akili yako ya juu – akili ya jamii, akili ya dunia- na akili iliyo ndani yako ya Knowledge. Hapa ndipo unakuwa moja katika sehemu zako zote. Hapa ndipo unaanzisha ufarisi wa uadilifu wako.
Hii ndio inakupatia nguvu na uwezo wa Mbunguni ukisafiri hapa duniani. Hii inakupatia madhumuni, maana na mwelekeo kwa kuwepo yako hapa na inatoa wito kwa watu fulani ambao watakuwa na jukumu muhimu katika ugunduzi na kuelezea lengo kubwa zaidi ambalo limekuleta hapa kwa wakati huu, katika hali hii. Hii ni hatima yako.
Usilalamike kuhusi dunia. Usiwe na uchungu au uchovu katika mtazamo wako wa dunia, kwa kuwa hii ndio dunia umekuja kutumikia. Ni kamilifu kwako. Hii ndio sababu umekuja.
Usiikane ama utakana dhamira yako kuwa hapa. Usiihukumu, ama utajihukumu pamoja nayo. Usijitenganishe kutoka kwake, ama utapoteza uhusiano na asili yako ya ndani.
Hatima imo nawe. Wito mkubwa unaenda nje. Mtume anatayarishwa kuongea duniani. Ufunuo Mpya umo hapa.
Ni baraka kubwa kuwa duniani katika wakati huu – wakati wa Ufunuo! Ni baraka kubwa kuwa unaweza kujifunza kuhusu haya. Ni baraka kubwa kuwa na hatima, kujifunza kuihusu na kuwa na unyenyekevu na hekima ya kuipokea.
Watu huwa na shida na mambo haya kwa sababu ya kiasi ambacho hao wanahusisha imani yao, malalamiko yao na mawazo yanayo wahusu, ambayo kwa mara nyingi hayana kitu chochote cha kufanya na swala linalotamkwa, ni nani hao kibinafsi na sabau yao kuwa duniani.
Mabadiliko ni magumu kwa watu, hasa mabadiliko ya ndani, lakini ni asili na lazima au huwezi kuishi maisha makubwa au ya lengo kubwa zaidi. Na huwezi kupatikana kwa mahusiano zaidi na muungano mkubwa na wengine.
Hii ndio malipo ya kiingilio. Hii ndio inamaanisha kupata jibu kwa maombi yako. Kwa kuwa maombi yako yakijibiwa inammanisha mlango umefunguliwa, na ni lazima uupitie. Sio safari ya maamuzi yako na haitatokea kulingana na maneno yako, mawazo na matarajio.
Ukitaka Mungu akusaidie, lazima basi umuwache Mungu akukusaidie na akuongoze. Mungu anakuongoza na anakusaidia kwa njia ya nguvu na uwepo wa Knowledge.
Lakini ni lazima uwe katika mahusianio na Knowledge, ukuchukue Hatua kwa Knowledge, ufarisi ukweli wake, uwezo wake kamilifu na kuendeleza ujuzi wa uvumilivu utaokuwa muhimu kwako kwa safari hii katika mikoa ya maisha na ufarisi ule kwa sasa hauko katika ya dhana zako au uelewa wako.
Mungu anakijua kile chakuja katika upeo wa macho. Swali ni, watu wanaweza kujibu na kujiandaa, na wanaweza kupokea maandalizi yale Muumba wa uhai wote ametuma duniani?
Ubinadamu hauwezi kijitayarisha. Haujui kwa nini unajitayarisha. Haujui hali ya maisha katika ulimwengu. Haujui jinsi ya kujitayarisha. Hautarajii kukabiliwa na dunia mpya.
Kwa hivyo haujajiandaa na hauna fahamu, unafikiri kuwa siku zijazo zitakuwa kama zamani, unaishi katika siku zilizopita, na kujihusisha na siku zilizopita, bila kuona hali ya mabadiliko ya dunia- mazingira ya inayobadilika na mabadiliko makubwa yanayokuja katika upeo wa macho.
Hamuna muda wa kutosha wa kutitayarisha kwa haya yote, kwa maana yako katika mwendo, na hamuwezi kuyazuia. Hamuwezi kuzuia kuingia katika dunia mpya. Hamuwezi kuzia dunia yenyu iibuke Jumuiya Kuu ya maisha katika ulimwengu. Maingilio tayari yameanza duniani kupitia jamii zilizo janja ambazo zipo hapa kupata faida kwa sababu ya ujinga wa binadamu na matarajio ya binadamu.
Hamuwezi kutoroka hatima yenyu, munaweza kuona, na hatima hii itawainua, au itwashinda, kulingana na jinsi mutajiandaa na uwezo wenyu wa kujibu – uwajibu wenyu.
Huu ndio wakati. Hamuna wakati wa kuwa wadhaifu. Hamuna wakati wa kujificha katika hisia kinzani. Hamuna wakati wa kujipoteza katika hobbies zenyu, mapenzi yasio ya dhamira na tafrija haribifu.
Dunia yabadilika. Inasonga chini ya miguu yenyu. Inatetemesha miji yenyu. Inanyima watu wenyu. Inabadilisha jinsi mutakavyoishi duniani. Inabadilisha hali ya anga duniani, hali ya hewa, mazingira,  uwezo wa kuzalisha chakula na rasilimali mutakazohitaji kudumisha utamaduni.
Ni nzito. Ni kubwa. Lakini watu bado wanalala, wanaota, wamepotea, hawaajibiki, wako obsessed, preoccupied, aliwasihi, na wanaamini kile wanachoambiwa na viongozi wale wanajua kidogo tu kuliko kile hao wenyewe wanajua kuhusu yale yajao katika upeo wa macho.
Lakini watu hawezi kuwa wajinga kabisa kwa sababu Knowledge inaishi ndani yao, na Knowledge inatoa ishara la onyo. Hii ndio maana watu wana wasiwasi. Hii ndio maana watu wanahisi ukosefu wa uhakika kuhusu uimara wa mustakabali wa binadamu. Hii ndio maana watu wana wasiwasi.
Wasiwasi hii ndio inakupatia kidokezo kwamba katika kiasi fulanu unakabiliana na Mawimbi Makubwa ya Mabadiliko yajayo duniani na badiliko la nafasi ya binadamu katika ulimwengu.
Ni ishara ya mabadiliko makubwa. Hauielewi. Hauwezi kuifafanua. Lakini uko hapa kukabiliana nayo kwa sababu ni hatima yako.
Kutoka upande mkubwa zaidi, kutoka upande wa Uumbaji, hatima ni kila kitu. Lakini sio hatime ile wewe mwenyewe umejiamulia. Ni hatima ile Mungu amekupatia. Ndio maana uko hapa. Ndio maana nafsi yako iko vile ilivyo. Ni kamilifu kwa wito wako wa kweli katika maisha, wito ambao una uwezekano bado haujautambua.
Hii ni hatima. Hii inaishi zaidi la eneo ya akili. Zaidi ya eneo la filosofia na theolojia, zaidi ya upendeleo, zaidi ya hofu, zaidi ya vivinyovinyo, zaidi ya uhakika wa binadamu- singizio la uhakika wa binadamu- zaidi ya imani ya dini, zaidi ya nafasi ya kisiasa, zaidi ya nadharia ya uchumi ni hatima.
Akili yako haitaelewa lakini katika sehemu ya ndani utaanza kujibu kwa sababu katika sehemu ya ndani, umeunganishwa na hatima.
Una hatima ya kukutana na watu fulani kama unaweza kuhitimiza mkutano huo, kama hautapotea njiani kwa  mkutano huu mkubwa na wengine.
Ni hatima kwamba lazima mukabili dunia mpya na ukweli wa Jumuiya Kuu ile Mungu atawafunilia kutumia Ufunuo Mpya.
Ni hatima kwamba unayasikia maneno haya. Ni hatima imeleta Ujumbe Mpya kwako na imekuleta kwa Ujumbe Mpya.
Hatimaye, utaelewa mengi ya mambo haya. Lakini kwa sasa, ni swala la kuwa na imani kubwa kwamba nguvu ya Knolwedge inaishi ndani yako, kwamba ni safi na ni uumbaji wa Mungu.
Ni unyenyekevu na utambuzi utakaoleta utakuwezesha kutambua tofauti kati ya Knowledge na mawazo, hofu na matarajio yako na mawazo, hofu na matarajio ya wengine.
Hapa ndipo unakuwa mjuzi. Hapa ndipo unaweza kutambua. Hapa ndipo hauko kama mtoto yule lazima aongozwe, bila kujua, kwa maana hii haitakuwa sahihi katika dunia mpya.
Ubinadamu lazima upevuke. Raia wake lazima wafahamu na wawe macho, watayarishwe na waimarishwe. Wacheni watoto wawe watoto, lakini kama wazima, lazima mupate mtazamo mkubwa na muwajibike.
Hizi sio nyakati za kale. Hauambiwi uwe kama kondoo. Unaambiwa ukabiliane na haya, na uchukue hatua kwa Knowledge na uruhusu Knowledge ifanye mabadiliko kwa maisha yako na ikufunulie hatima yako kubwa.
Hii ndio Nia ya Mbinguni, na sas lazima iwe nia ya binadamu.